Polygamy galore: Tazama watu mashuhuri katika ndoa za zaidi ya mke mmoja

Ndoa za zaidi ya mke mmoja zimekuwa  zikizua mijadala mikali lakini siku hizi, huenda makali ya pingamizi ya ndoa hizo sasa yamepungua na hata watu mashuhuri wanajipata katika ndoa hizo huku wengi wakikubali kuwa  mke wa pili, wa tatu au hata wane. Baadhi yao walijiingiza katika ndoa hizo kwa hiari ilhali wengine walijipata ndani kwa ajili ya kuaga dunia kwa wake wa kwanza wa waume zao. Hii hapa orodha ya watu unaowajua katika ndoa kama hizo.

1.Suzanna Owiyo

Mwanamuziki huyu mashuhuri wa Kenya ni mke wa pili wa Ounga Oguda kwa miaka 16 sasa. Owiyo ana mtoto moja

  1. Esther Passaris

Mwakilishi huyu wa akina mama Nairobi ni mke wa pili wa mfanyibiashara na mkulima mashuhuri  Pius Mbugua Ngugi.

  1. Lilian Ng’ang’a

Lillian Ng’ang’a  ni mke wa pili wa gavana wa machakos Alfred Mutua. Wawili hao hawajapata mtoto. Mutua ana mke wa kwanza  Josephine Thitu Maundu.

  1. Mary Kilobi

Mtangazaji huyo wa KTN ni mke wa tatu wa mkuu wa COTU Francis Atwoli. Atwoli hajaficha kwamba  ana wake wengi .

  1. Mama Ngina Kenyatta

Mama wa kwanza wa taifa  alikuwa mke wa nne wa rais wa kwanza Jomo Kenyatta.   Orodha ya wake za baba wa taifa  ni hii.

Mke wa kwanza Grace Wahu – 1919

Mke wa pili - Edna Clarke -1942-1946

Mke wa tatu- Grace Wanjiku – 1946- 1950

Mke wan ne  – Ngina Kenyatta (Mama Ngina) -1951-1978

  1. Sabina Chege

Mwakilishi huyu wa akina mama wa  Muranga  ni mke wa pili wa aliyekuwa mkuu wa bodi ya maziwa nchini  Gathitu Maina.

  1. Jacquline Mengi

Mrembo huyo wa Tanzania na mwanamuziki alikuwa mke wa marehemu bilionea Reginald Mengi aliyeaga dunia Mei mwaka jana. Ana watoto wawili mapacha

  1. Cate Waruguru

Mwakilishi huyo wa akina mama wa Laikipia  alikiri kuhusu ndoa yake kwa wakili  William Kigen kupitia mahojiano katika runinga ya KTN. Alieleza kwamba hana soni kukiri kwamba ni mke wa pili na kwamba ana fahari sana  ya kuwa na mume wake.

 “ Unagundua kwamba mwanamme huyu ndiye nayetaka kuwa naye. Nataka aliye na ujasiri athubutu kunilaani kwamba  nitaenda motoni kwa kuwa mke wa pili."

Aliwashauri wanawake kuelewa kwamba mwanamme ni wako tu wakati upo naye .

 “ Mume wa mtu ni wake anapokuwa nyumbani. Mzee wa boma akishatoka, jitunze na uchague unachotaka katiba inaruhusu ‘ alisema Waruguru

  1. Yvonne Okwara

Mtangazaji huyu wa runinga ya Citizen  ni mke wa pili wa  Dr Andrew Matole.

Kulingana na duru, kabla ya harusi yao eneo la harusi lilibadilishwa mara kadhaa pakizuka hofu kwamba mke wa kwanza alikuwa amepanga kuikatiza harusi hiyo.  Matole alikuwa na mke wa kwanza Alice  Manyole ambaye wamepata watoto watatu naye.

  1. Emmy Kosgei

Emmy Kosgei  yupo katika ndoa ya zaidi ya mke moja baada ya kushawishiwa kufunga pingu za maisha na mhubiri kutoka Nigeria  Anselm Madubuko  muda mfupi baada ya kukutana huko Mombasa.

Emmy na  Anselm  walioana mwaka wa 2013 baada ya mke wa kwanza wa  raia huyo wa Nigeria  Connie Uzuoamaka Madubuko kuaga dunia mwaka wa 2012.