Riyad Mahrez aipeleka Algeria kwenye Fainali za Afcon

Senegal itachuana na Algeria kwenye finali za Afcon tarehe 19 mwezi huu. Senegal ilibandua Tunisia baada ya kuicharaza goli moja bila jibu. Mchezo huo ulijawa na matukio mengi huku mechi ikishudia penalti mbili.

Ferjani Sassi alipoteza mkwaju wa penalti baada ya Kaidou Koulibaly kunawa mpira kunako dakika ya 73.

Dakika chache baadaye, Henri Saivet alipoteza penalti yake pia upande wa senegal jambo lililolazimisha mchezo huo kwenda muda wa nyongeza.

Kilio kilianguka upande wa tunisia baada ya Dylan Bronn kujifunga mnamo dakika ya 100 na kuwapa Senegal tiketi ya kucheza fainali ya Michuano hiyo.

Riyad Mahrez alicheka na wavu mnamo dakika ya 93 kuwainua mashabiki wa Algeria. William Troost-Ekong alitia mpira wavuni wake kuipa Algeria uongozi mnamo dakika ya 40.

Idion Ighalo alisawazishia Nigeria mnamo dakika ya 72 kupitia tuta loa penalti baada ya Aissa Mandi kunawa mpira.

Kufuatia matokeo hayo, Algeria itakabana koo na Senegal mnamo tarehe 19 mwezi huu huku Nigeria ikigaragazana na Tunisia kuwania nafasi ya tatu mnamo tarehe 17 mwezi huu.