Staa wa soka Paul Pogba afunguka kuhusu dini yake

Staa na nguli wa soka kutoka nchi ya Guinea, Paul Pogba na ambaye anaichezea timu ya Manchester United katika ligi ya Premier na timu ya kitaifa ya Ufaransa amefunguka na kusimulia jinsi alivyobadili dini yake na kuwa muislamu.

Mchezaji huyu wa kati amechapisha picha akiwa katika Mecca mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Nyota huyu wa kimataifa anasimulia jinsi alivyokuwa akijiuliza maswali kichwani kuhusu maswala yanayohusu dini hatimaye akajipata katika dini ya kiislamu.

katika mahojiano ya kipekee na The times New Life, Pogba amefunguka kuwa dini ya kiislamu ni

" Ni kila kitu kwangu. Inanifanya niwe mkamilifu na huru kwa kila kitu."

"Ni mabadiliko mazuri maishani mwangu kwa sababu sikuzaliwa muislamu na mamangu mzazi Nilikuwa nikiwahehimu watu.' aliongezea kusema.

"Maisha yana majaribio mengi. Kwa mfano, kwa sasa nipo nawe hapa, huenda ikawa wewe sio muislamu ila wewe ni binadamu wa kawaida. Una uhusiano wa kibinadamu na heshima kwa jinsi ulivyo, dini unaypifuata, rangi ya ngozi na kila kitu." aliongeza kusema Pogba.

Hadithi imehaririwa na kuchwapishwa na Abraham Kivuva