Steven Pollack achukua hatma za ukufunzi Gor Mahia

EBXgQ2cX4AAWOwv
EBXgQ2cX4AAWOwv
Klabu ya Gor Mahia inatarajia kumtangaza aliyekuwa kocha wa Asante kotoko Steven Pollack kama mkufunzi wao mpya hapo kesho baada ya aliyekuwa kocha wao Hassan Oktay kujiuzulu na kurejea kwao nyumbani kwa madai ya kifamilia.

Pollack anatarajiwa kuiongoza K'ogalo kwenye mechi ya Caf Champions League kule nchini Burundi siku ya jumammosi kama mechi yake ya kwanza.
Mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachie amesema kuwa Pollack alikuwa mmoja wa makocha walioandika barua za kuitaka nafasi iliyoachwa naye Darren Kerr ila alikuwa katika nafasi ya tatu kwenye matokeo ya mahojiano.

Awali, Steven Pollack alikuwa mkufunzi wa Asante Kotoko, Inter Turk ya Finland pamoja na Berekum Chelsea ya Ghana. Pollack mwenye umri wa miaka 58 anatarajiwa kutia sahihi mkataba wa miaka miwili na mabingwa hawa wa Kenya.