Timu ya Raga ya 7s ya kina dada yafaulu kushiriki Olimpiki 2020

Kenya
Kenya
Timu ya  raga ya 7s ya kina dada imejipatia tiketi ya kushiriki katika Olimpiki ya Tokyo Japan 2020, baada ya kufuzu katika  fainali ya mashindano hayo nchini  Tunisia Jumapili.

Kenya ambao  ni mabingwa watetezi waliwapiga  wenyeji Tunisia 19-0 kwenye  michuano ya nusu finali  na  kujikatia tikiti  ya moja kwa moja kwenda Japan

Timu hiyo ya Kenya, maarufu kama Lionesses ilikuwa timu ya nane kufuzu kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020.

Brazil  itawakilisha Amerika kusini huku  Ulaya ikiwakilishwa na  Uingereza ambao walifuzu katika michuano hiyo.

Ikiongozwa na kocha Felix Oloo, Lionesses   walisambaratisha Zimbabwe kwa kushinda 26-5, 36-0 dhidi ya Ghana na kuwapiku Botswana  Jumamosi kwa 49-0