uefa

Ubashiri wa ligi ya mabingwa Ulaya

Raundi ya nne ya ligi ya mabingwa Ulaya utasakatwa leo usiku huku klabu mbali mbali zikitarajia kuandikisha ushindi ili wafuzu katika mkondo utakaofuata.

Chelsea vs Ajax

Vijana wake Frank Lampard watakuwa wanawakaribisha Ajax nyumbani kwao Stamford Bridge. Wana Chelsea waliweza kuwapiga Ajax bao moja kwa bila katika uwanja wao Johan Cruijff.

Klabu hizo zinatarajia kupata ushindi usiku wa leo kwani kwa sasa wote wanashikilia nambari moja katika kundi H kila mmoja akiwa na pointi 6.

Utabiri wangu Cheslea 2 Ajax 1.

Viongozi wa Tharaka nithi wapinga matokeo ya sensa

mount

Barcelona vs Slavia Praha

Wana Catolonia watawakaribisha klabu ya Slavia nyumbani kwao Camp Nou. Mkufunzi wa Barcelona ana uhakika kuwa vijana wake watamaliza washindi katika mchuano huo.

Barcelona wanaongoza katika kundi F na pointi 7 huku Slavia Praha wanashikilia nambari nne katika kundi hilo na pointi 1.

Utabiri wangu Barcelona watashinda kwa mabao 4 kwa 1.

barca

Liverpool vs Genk

Klabu ya Genk itasafiri hadi uwanjani Anfield nyumbani kwao Liverpool huku wakitarajia kuandikisha ushindi kama sio kutoka sare kwani klabu hiyo inashikilia nambari nne katika kundi E wakiwa wamepata ponti 1 huku Liverpool wakiwa nambari ya pili na pointi 6 nyuma yao Napoli ambao wanatawala kundi hicho kwa sasa.

Jurgen Klopp anaamini kuwa wachezaji wake wataweza kushinda katika mchuano huo.

Utabiri wangu ni Liverpool watashinda mechi hiyo kwa mabao 4 kwa 1.

genk

PATANISHO: Ukali wa mke wangu ulinipelekea kubugia pombe

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments