uholanzi (1)

Uholanzi kumenyana na Ureno katika fainali ya kombe la ligi ya mataifa

Uholanzi ilitoka nyuma na kuinyuka Uingereza mabao 3-1 katika nusu fainali ya kombe la Ligi ya Mataifa na kufuzu kwa fainali ambako watakutana na Ureno, ambao pia waliwanyuka Uswizi 3-1 katika nusu fainali ya kwanza, mabao ambayo yalifungwa na staa wa Juventus, Cristiano Ronaldo.

Real Madrid imekubali kumnunua Eden Hazard kwa pauni milioni 88

Uingereza walichukua uongozi kupitia kwa mkwaju wa penalty wa Marcus Rashford katika kipindi cha kwanza, kabla ya mlinzi Matthijs de Ligt kusawazisha.

Masihara ya safu ya ulinzi ya Uingereza yalipelekea Kyle Walker kujifunga mwenyewe, kabla ya kosa la Ross Barkley kumpa Quincy Promes fursa ya kufunga bao la tatu.

Fainali hio itachezwa Ureno siku ya jumapili hii katika mji wa Guimaraes.

PATANISHO: Unikome! Utapata mke mwingine anayependwa na mamako

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments