Uko na umama na wewe ni mwanamume,Shenzi sana ! Willy Paul amzomea Ringtone Apoko

Ringtone-vs-Willy-Paul
Ringtone-vs-Willy-Paul
NA NICKSON TOSI

Willy Paul kwa muda amekuwa akivumilia madhila ya matusi kutoka kwa msanii wa humu nchini Ringtone Apoko na mara hii hakuvumilia matusi kutoka kwa msanii huyo bali aliamua kumjibu papo hapo kama mwanamume.

Hivi maajuzi, Pozze kama anavyofahamika, ametoa wimbo mpya akimshirikisha msanii Nadia Mukami, wimbo ambao kulingana na Ringtone umekosa maadili kwa kile anasema Willy Paul anaharibu jina la Mungu na wasanii ambao wanafanya  miziki ya injili.

Katika posti tulizoziona za Willy Paul ambaye amekiri kuwa hupokea matusi ya kila mara kutoka kwa Ringtone, yeye hana umama kama Ringtone ambaye anapenda kubayuka mitandaoni.

Pozze alimtaka Ringtone kutoa wimbo mpya na kuona iwapou tafanya vyema kama wimbo alioutoa na Nadia.

Akimkashifu Apoko, Willy aliandika hivi katika mtandao wake japo maneno yaliyotumika hayana uhusiano na mwandishi ama kituo hiki.

“MATAKO WEWE RINGTONE @ringtoneapoko THE FACT THAT NIMETULIA ISIFANYE UONE KAMA MIMI NI UR FELLOW WOMAN!!! BLOODY NA UACHANE NA NADIA MUKAMI.. TOA WIMBO YAKO TUONE SHENZI, #NIKUNE IS A HIT AND UR LIFE IS A MISSSSS!!” alisema Willy Paul.

Wadau mpo?  Willy Paul ni mkali kuliko Diamond, Asema Ringtone

Hapa ni video ya Ringtone aliotuma kwenye mitandao ya kijamii na kumkashifu Pozze.

Baada ya kutundika video hiyo kwenye kurasa zake, Ringtone alifuatisha ujumbe ufuatao

“Niaje wakenya, leo nataka niseme I’m very disappointed. Yaani nimekasirika na kijana mmoja ambaye alikuwa anajifanya ni kijana wa Yesu ambaye anaitwa Willy, Willypozze. Willy Paul unaimba na Nadia Mukami kitu gani hio? Unataka kukuna wasichana ukunwe. Willy kukunwa unamaanisha nini kwa sababu wewe ulikuwa mtu wa kuwekelea watu mikono na sahii unaingiza wasichana mikono. It’s a shame. Nadia Mukami we are very disappointed wewe pia unataka kukunwa, unataka Willy akukune jamani. Mungu awasamehe Willy na Nadia Mukami,” aliandika Rintone.