United yailaza Derby, Uingereza yapiga marufuku kusalimiana kwa wachezaji

kusalimiana
kusalimiana
Manchester United ililaza Derby county 3-0 katika raundi ya tano ya kombe la FA na kunyakua tikiti ya mwisho ya robo fainali.  Luke Shaw alifunga bao la kwanza kunako dakika ya 33 huku Odion Ighalo akiongeza mawili katika dakika ya 41 na 70 na kukamilisha kichapo hicho.

Mfungaji bora wa Mancheter United katika historia ya klabu hio Wayne Rooney ambaye anachezea Derby alikua karibu kufunga kupitia mikwaju ya adhabu lakini kipa wa United Sergio Romero alihakikisha hakukua na goli la kufuta machozi. United sasa itacheza dhidi ya Norwich katika robo fainali baadae mwezi huu.

Wasimamizi wa ligi ya Uingereza FA wamepiga marufuku kusalimiana kwa wachezaji na maafisa wa mechi za ligi ya Uingereza kuanzia wikendi hii, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Haya yanajiri baada ya serikali kuwataka waweke mikakati ya kupambana mchipuko wa janga hilo ambalo linatishia kusambaa kote duniani.

Mshambulizi wa Real Madrid Eden Hazard amefanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu, na anazidi kupata nafuu. Mbelgiji huyo ambaye alijiunga na  Los blancos kutoka Chelsea mwanzoni mwa msimu huu alijeruhiwa wakati walipoteza 1-0 dhidi ya Levante mwezi Februari.

Hio ilikua mechi yake ya pili tu baada ya kupona jeraha lingine mwezi wa Januari. Haijulikani atarejea lini lakini madaktari wanaamini huenda asicheze tena msimu huu.

Uwanja wa Kasarani utafungwa ili kufanyiwa ukarabati mwezi huu, ili kuwa tayari kwa mbio za vijana wasiozidi umri wa miaka 20 mweji Julai 2019.  Kenya iliandaa mbio za kinda wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka wa 2017 na wananuia kuandaa mbio za kufana tena. Waziri wa michezo Amina Mohammed anadai serikali imeweka mikakati kabambe kuhakikisha wanaendeleza rekodi nzuri ya kuanda michezo nchini.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kanemwenye umri wa miaka 26, atafikiria kuhamia Manchester United msimu huu. Kane hana mpango wa kutia saini mkataba mwingine na Tottenham. Kwingineko Arsenal wanaweza kufungua njia kwa John Stones, kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu.