wanyama__1575116037_23539

Victor Wanyama awindwa na Hertha Berlin ya Ujerumani

Kocha wa Hertha Jurgen Klinsmann anataka kusajili kiungo mkabaji na anasuka mipango ya kumnasa kiungo wa Kenya na Tottenham Victor Wanyama, 28. (Telegraph)

Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 27, yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Hertha Berlin juu ya uwezekano wa usajili mwezi ujao utakaompeleka ligi ya Bundesliga. (ESPN)

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anataka kuihama Arsenal kwa udi na uvumba. (Mirror)

Manchester City na Manchester United wanakumbana na ushindani kutoka Liverpool, Real Madrid na Barcelona kumsajili kiungo Mjerumani Kai Havertz, 20 kutoka Bayern Munich. (Sun)

Manchester City walishtushwa na tangazo rasmi la Arsenal kumteua Mikel Arteta kuwa kocha wao mpya kupitia runinga na mitandao ya kijamii. (Mail)

Mikel Arteta

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola amethibitisha kuwa kiungo huyo wa Ufaransa mwenye miaka 26 anataka kusalia Manchester United na “kushinda mataji”, lakini anahitaji uungwaji mkono zaidi kutoka klabuni. (Telegraph)

Raiola pia amesema kuwa “anajisikia vibaya” kushindwa kuwaunganisha Pogba na kocha Mfaransa wa Real Madrid Zinedine Zidane katika dirisha lililopita la usajili. (Star)

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments