(+ Video) Taarifa za vifo katika runinga ni baraka, muhudumu wa mochari aeleza

Screenshot from 2019-11-28 14-58-45
Screenshot from 2019-11-28 14-58-45
Geofrey Mwakorongo kutoka wodi ya Chala wodi kaunti ya Taita Taveta

amefunguka A-Z jinsi anavyoendesha kazi yake ya mochari.

Katika video inayotamba kwenye mitandao ya kijamii, mwanaume huyu anadokeza waziwazi bila kuogopa jinsi kazi ya mochari inampa pato kubwa.

Tazama video:

https://www.instagram.com/p/B5aGGxZAQIQ/

"Mimi nafanya mochari hapa Voi. Kazi hii nimerithi kwa ukoo wetu. Watu kwetu wanafanya mochari..." Alianza kufunguka.

Alipoulizwa kuhusu changamoto za kazi hii,

"Hii kazi inalipa siwezi sema ikona changamoto japo tunakuwa na losses kama watu hawakufi..." Alisema Geofrey.

"Ata kama iko ni kidogo kidogo, tuseme tunakuanga na losses time watu hawakufi..." Asisitiza Mwakorongo.

Mwanamume huyu alisema kuwa sio kila mwezi kazi ya mochari inakuwa nzuri,

"Na kunakuanga na upper season kwanza msimu huu wa Disemba watu wanadondoka sana na pia Aprili, Agosti na Disemba ni peak ya biashara yangu." Mwakorongo amesema.

Mwakorongo amesema kuwa taarifa za mauti katika runinga huwa ni habari njema kwake,

"Saa hii ukiskia TV watu 10 wamekufa kwa breaking news tunashukuru mungu..."

Mwakorongo tayari ashaanza mipango imara ya kujipanga msimu huu wa Disemba,

"Tunapoongea saa hii nimenunua redio,nikona baiskeli,napanga kuongeza mke kwa sababu ya hii kazi..."

Kwa sababu kazi nyingi Mwakorongo ameweka wazi kuwa atafungua matawi katika sehemu tofauti,

"Halafu sasa nafungua tawi nyingi kwa sababu watu wanakufa sana.Nataka nifungue Mwatate,nifungue Buguta,nifungue na Taveta.."

Aidha, mwanamume huyu ametoboa siri ya kazi yake,

"Ni kazi na ambayo inalipa. Halafu siri kubwa sana. Unaona kazi yangu ya mochari,kwa nini inaendelea? Huwa natoa sadaka kasisi anaombea biashara yangu inanoga..."

Amesema kuwa juhudi zake za kutoa sadaka zinaongeza pia kazi,

"Jinsi ninavyozidisha kutoa sadaka, vifo vinaongezeka. Lazima mtu awekeze kwa kanisa kupitia sadaka ili biashara iwe nzuri..."

Mwakorongo hawakuwaacha nyuma wagonjwa ambao ni mahututi,

"Na ukiona wewe ni mgonjwa unataka kufa you pay..."