Patanisho: 'Kakangu alinichapa baada ya kuchapa mtoto wake mgonjwa, naomba anisamehe'

“Nilimpiga mtoto wa kakangu ambaye amekuwa akigonjeka, kakangu akaja tukaanza kugombana hapo akanichapa, sasa ile hasira nikatoka kwa boma nikaondoka,” Joyce alisema.

Muhtasari

• Joyce alisema kwamba walikosana na kaka yake mwezi Machi 2022 baada ya kumuadhibu mtoto wa kakake huyo.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho kwenye Radio Jambo, Gidi na Ghost asubuhi, mrembo Joycemwenye umri wa miaka 24 aliomba kupatanishwa na kakake mkubwa, Joseph mwenye umri wa miaka 42.

Joyce alisema kwamba walikosana na kaka yake mwezi Machi 2022 baada ya kumuadhibu mtoto wa kakake huyo.

Joyce alisema kwamba amegundua alifanya makosa kwa kumchapa mtoto wa kakake ambaye alikuwa mgonjwa, jambo ambalo lilizua uhasama mkubwa baina yao kiasi kwamba kakake akakomesha mazungumzo naye hadi sasa.

Mrembo huyo alisema kwamba kwa sasa yeye yuko Mombasa na kakake yuko nyumbani sehemu za Kabras.

“Nilimpiga mtoto wa kakangu ambaye amekuwa akigonjeka, kakangu akaja tukaanza kugombana hapo akanichapa, sasa ile hasira nikatoka kwa boma nikaondoka,” Joyce alisema.

Joseph alipopigiwa simu, alisema kwamba mahali alikokuwa wakati anapigiwa simu hangeweza kuzungumza kwani alikuwa kazini.

“Nimekubali msamaha wake,” na kumaliza tu bila maneno mengi.

Joyce alishukuru Radio Jambo kwa kuweza kumpatanisha na kakake na kusema kwamba baadae atamtafuta ili waweze kuzungumza.