Visa vya coronavirus nchini Kenya vyatimia 607

EASTLEIGH
EASTLEIGH
Kenya imesajili visa 25 zaidi vya maambukizi ya virusi vya corona na kufikisha idadi ya jumla ya watu 607 waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Katibu msimamizi katika wizara ya Afya Rashid Aman alisema kwamba kati ya 25 hao wakenya ni 22, Tanzania mmoja, Uganda mmoja na Uchina mtu mmoja.

Soma pia:

Nairobi iliongoza kwa jumla ya watu 17 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona katika muda wa chini ya saa 24, huku kaunti ya Isiolo ikiwa kaunti ya hivi punde kusajili kisa cha corona kufikisha 18 kaunti ambazo zimesajili maambukizi ya corona kote nchini. Mtaa wa Eastleigh katika kaunti ya Nairobi umesajili visa tisa ya maambukizi.

Aman alitangaza kwamba watu watatu zaidi wamefariki kutokana na virusi vya corona katika kipindi cha chini ya saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya walioaga dunia kutokana na covid 19 humu nchini hadi watu 29.  Aman pia alisema jumla ya watu 197 wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya watu saba zaidi kupona ugonjwa huo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Serikali pia imengaza kwamba imekamilisha mipango ya kuwarejesha nchini wakenya wote waliokuwa wamekwama nchini India na ambao walikuwa nchini humo kwa matibabu. Katibu msimamizi wa Afya Rashid Aman amesema ndege iliyobeba wakenya hao inatarajiwa nchini leo (Alhamisi).

Soma pia:

Wakati huo serikali imetangaza kwamba agizo la kutotoka nje na kuingia katika mitaa ya Eastleigh hapa Nairobi na Oldtown, Mombasa halikunuia kudhulumu yeyote bali ni kudhibiti usambaaji wa virusi vya corona. Ametoa tahadhari kwa baadhi ya watu wanaoruhusu jamaa wao kutoka maeneo haya na kuishi nao wakati huu akisema kwamba hatua hii inahatarisha maisha ya familia zao.

Soma pia;