VAR ilikuwa na matukio sabini kwa ujumla wikendi hii.
VAR inatumika kuangalia iwapo mchezaji anastahili kadi nyekundu au hafai, iwapo faulo inafaa kuwa penalti ama mchezaji mwingine alidanganya pamoja na kuyakubali magoli au kuyakataa kutokana na kuotea kwa mchezaji, kucheza vibaya na hata kunawa mpira kabla hujaingia wavuni.
Kwenye mechi zingine, goli lake Ashley Barnes lilikataliwa na VAR baada ya kugundulika kwamba Chris wood alikuwa ameotea. Wolves kwa upande mwingine ilishuhudia goli lao limekataliwa na VAR ugani King Power Stadium baada ya Leander Dendocker kunawa mpira kabla hajacheka na wavu.
Roberto Pereira wa Watford alinyima penalti baada ya Glen Muray wa Brighton kunawa mpira. Hata hivyo, VAR iliamua kuwa haikustahili penalti kwani ilisemekana kuwa Muray hakunawa akitaka.
VAR imeibua maswali mengi hasa kutoka na mashabiki huku kocha wa Wolves, Nuno Santos akisisitiza kuwa VAR inaharibu mchezo licha ya kuleta usawa ndani yake.