Wachezaji ghali waliosajiliwa nchini Uingereza msimu huu

Dirisha la uhamisho lilikamilika hio jana na huku hilo likifanyiaka kunazo klabu zilizotoa mkwanja mrefu kuongeza talanta klabuni mwao msimu huu pamoja na kuziba mapengo yaliyoachwa wazi.

Arsenal, Everton na Totenham ni baadhi ya vilabu zilizohusika kwenye biashara za maana kwenye dirisha la uhamisho lililokamilika hio jana jioni huku kwa ujumla ligi hio ilishuhudia billioni moja nukta nne zikitolewa kwenye akaunti za vilabu zao.

Harry Maguire

Mlinzi huyu wa kati alijiunga na manchester United akitokea Leicester City kwa kima cha pauni millioni themanini na tano. Maguire mwenye umri wa miaka 26 alitia sahihi mkataba wa miaka sita.

Nicolas Pepe

Nicolas pepe alijiunga na Arsenal akitokea klabu ya Lille iliyoko nchini Ufaransa kwa ada ya millioni sabini na mbili. Winga huyu anayetokea taifa la Ivory Coast alitia sahihi mkataba wa miaka mitano na Arsenal.

Tanguy Ndombele

Klabu ya Totenham Hotspurs ilitumia pauni millioni sitini na tatu kumchukua kiungo wa ufaransa na Lyon, Tanguy Ndombele mwenye umri wa miaka 22. Ndombele ametia sahihi mkataba wa miaka mitano ugani White hart Lane.

Rodri

Manchester City ilimsajili kiungo wa Atletico Madrid na uhispania, Rodrigo kwa kima cha pauni millioni 58. Rodrigo ni kiungo mkabaji mwenye umri wa miaka 23 na alitia sahihi mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Uingereza.

Aaron Wan Bissaka

Muingereza huyu alitokea klabu ya Crystal Palace msimu uliopita na alihusika na mechi 32 huku akiongoza kwa kuwa mlinzi aliyewapokonya washambulizi mpira mara nyingi. Bissaka alitia sahihi mkataba wa miaka mitano ugani Old Trafford.

Manchester United ilitumia jumla ya pauni 148 millioni huku ikifuatwa na Aston Villa kwa pauni millioni 144. Arsenal ilichukua nafasi ya tatu kwa kima cha pauni millioni 138 huku Manchester City ikitumia kima cha pauni millioni 134. Baada ya kumsajili Tanguy Ndombele, Totenham ilikamilisha tano bora kwa utumizi wa millioni 111 sawia na Everton iliyokamilisha usajili wake Alex Iwobi.