EBg_kFMWsAAT_Ak

Wachezaji waliopatikana na hatia ya ubakaji kuzuiliwa kwa wiki moja zaidi

Wachezaji wawili wa raga, Frank Wanyama na Alex Mahaga waliopatikana na hatia ya kumnajisi mwanamziki mmoja mwaka uliopita watazuiliwa kwa wiki moja zaidi kutoka sasa hadi tarehe 16 mwezi Agosti wakingoja kupokea hukumu yao. Frank na Alex walimnajisi mwanamziki huyo baada ya sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake.

Rugby Players Alex Mahaga and Frank Wanyama during a court appearance.

Wakili wa washatkiwa anasema kuwa mwanamke aliyenajisiwa (24) ni mtu mzima hivyo alipaswa kuwa na uwezo wa kuwazuia wawili hao kutomfanyia kitendo hicho kwani wawili hao wana umri wa miaka 23 na 22.

Hata hivyo mwanamziki huyo alisema hakuwa na uwezo wa kuzuia wawili hao.

KWALE: Wanafunzi wapewa dawa za uzazi wa mpango kuzuia mimba

 “Mie singeweza kupigana na wanaume wawili hasa ikizingatiwa kwamba wanacheza mchezo wa raga kama taaluma yao hivyo walikuwa na nguvu nyingi kuniliko. Kwa kuwa sikuwa na uwezo, ilinibidi niwaachie wafanye watakalo,” alisema mwanamziki huyo.

Pamoja na hayo, mwanamziki huyo anasema kuwa hangeweza kwenda kuzungumza na polisi kwani alihofia maisha yake pamoja na kuhofia kwamba huenda asipate usaidizi kutoka na kuwa mmoja wa wawili hao ana jina ‘kubwa’.

Pia, alijaribu kumweleza Wanyama baadaye kuhusu hali hio ila mchezaji huyo alifikiria kuwa mwanamziki huyo alikuwa anahitaji pesa zake. Wanyama alimfukuza na kumtaka aje na wakili kwa ajili ya suala hilo.

Askari wa kaunti ya Busia wapatikana na hatia ya kuwajeruhi wanahabari

Baada ya kupatikana na hatia, mawakili wao, Wafula simiyu na Ombui Ratemo waliomba mahakama kutowafunga nyumbani kwani walikuwa na majukumu ya kuendeleza masomo yao pamoja na kuliwakilisha taifa katika mchezo wa raga.
Wanyama kwa sasa ni mchezaji wa Helsinki ya Philadephia huku Mahaga ni mchezaji wa Kenya Harlequins.

Awali mwaka huu mwezi julai,J aji Martha Mutuku alikuwa tayari kutoa hukumu ya wawili hao ila akasitisha kwani Mahaga hakuhudhuria koti siku hiyo kwa madai kuwa yeye ni mgonjwa.

Wakili wa mshatki ameitaka mahakama kuwafunga wawili hao kufungo cha miaka kumi na mitano ama kuwapa kifungo cha maisha gerezani.

“Ubakaji ni jambo mbaya sana. Mtu hapaswi kumtumia mwenzake vibaya kwa madai ya jinsia yake ama kwa vyovyote vile,”Wakili wake mwanamziki huyo.

SOMA MENGI HAPA

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments