Wachezaji wanne wa Sampdoria wapatikana na corona

9c28f4ae85fa143392edb22a23a9cb3247540db3
9c28f4ae85fa143392edb22a23a9cb3247540db3
NA NICKSON TOSI

Klabu inayoshiriki ligi kuu ya Serie A Italia imethibitisha kuwa wachezaji wao 4, akiwemo mmoja aliyekuwa amepona dhidi ya virusi vya Corona wameambukizwa virusi hivyo hatari.

Klabu hiyo imesema kuwa visa hivyo viligunduliwa baada ya wachezaji kufanyiwa vipimo.

“During the tests to which the footballers were subjected, three new cases of COVID-19 emerged, with one player testing positive again,” imesoma taarifa kutoka Sampdoria .

Vilabu vingi vya Italia vinaendelea kuwapima wachezaji wao kama maandalizi ya kujianda kuendeleza msimu wa ligi uliositishwa baada ya mkurupuko wa virusi hivyo.

Yakijiri hayo pia, klabu ya Fiorentina nayo imetangaza kuwa wachezaji wake watatu pia wameambukizwa virusi hivyo.

Kufikia sasa, wachezaji wanane katika ligi hiyo ya Serie A wameambukizwa virusi hivyo baada ya klabu ya Torino kusema mmoja wa wachezaji wake walikuwa waathiriwa.

Wachezaji wa Fiorentina waliopatikana na virusi hivyo ni Patrick Cutrone, German Pezzella na Dusan Vlahovic.

Kutokana na visa hivyo sasa usimamizi wa Fiorentina umesema kuwa wachezaji waliosalia watafanyiwa vipimo leo .

Uongozi wa Serie A ulikutana na serikali ya Italia kubaini iwapo ligi hiyo itarejelea viwango vyake vya kawaida baada ya kusitishwa kutokana na janga hilo lililoathiri taifa hilo pakubwa.