Waihiga Mwaura atoa ushahidi kuhusu matukio ya Olimpiki

Wahiga Mwaura amedhibitisha kuwa mwaka wa 2016 kwenye mashindano ya olimpiki, kulikuwa na ufisadi ulitekelezwa na maafisa wasimamizi wa 'Team Kenya'.

Wahiga Mwaura ni mwanahabari wa michezo ndani ya runinga ya Citizen.

Mwaura alisema kuwa hakupata ufadhili wowote wa malazi au hela za kukidhi mahitaji yake wakati alikuwa Rio nchini Brazili kutoka kwa kamati ya Michezo nchini. Aliongeza kuwa hakufanya mazungumzo yoyote na vinara wa kamai ya michezo wakati huo.

"Nilifahamu uwepo wa orodha ilyokuwa na mipango ya kwenda Rio. Jina langu lilikuwepo. Baadaya kurejea nchini kutoka Rio, Niliandika habari kuhusu matukio hayo huku nikiita habari hio 'Rio Fiasco'," Mwaura alitoa ushahidi mbele ya hakimu  wa mahakama ya milimani Elizabeth Osoro.
Mwaura alisema kuwa hakujua jambo lolote kuhusu shilingi elfu mia moja alizokuwa amadikiwa keshapata kwenye orodha hio.
"Malazi yangu na mahitaji yangu yalilipwa na mwajiri wangu pamoja na ya wanahabari wezangu niliokuwa nao. Ningependa kusema kuwa baada ya kurejea humu nchini,ckupata ufadhili wowote kutoka kwa NOCK wala serikali yenyewe." Mwaura alisema.

Aliyekuwa katibu mkuu wa michezo Hassan Wario pamoja na maofisa wengine wa tume iliyokuwa inashughulikia maswala ya Rio inakibiliwa na kesi ya ufisadi wa shillingi millioni 55 zilizofaa kutumika kuitayarisha 'Team Kenya'.