Waru vs Salamu! Mamia ya wakenya wafurahishwa na patanisho

Kuanzia kwa watangazaji Gidi na Ghost hadi kwa mamilioni ya mashabaki wa Gidi na Ghost asubuhi, kila mmoja amekubali kuwa kitengo cha leo cha patanisho kiliweza zaidi!

Yaani patanisho ya leo ndio iitwayo, baab kubwa, ya kukata na shoka, yenye mgurumo mkuu kuliko wa simba.

Hii ni baada ya watangazaji hao wawili kuweza kuwapatanisha Agnes Njeri na mumewe Basil ambaye alikuwa ametishia kuasi ndoa yake na kurudi nyumbani kwa Uganda.

Mwanadada Njeri, ndiye aliyesisimua patanisho ya leo huku akidai alimgeuza mumewe ambaye alikuwa anafanana na mwizi na kumrembesha na sasa hivi anafanana na MCA.

Waskizaji walimpenda kwa uwazi wake na ucheshi mwingi huku wakisema kuwa kwa kweli mwanamke akipenda amependa.

Njeri alisimulia jinsi alibidi apigane na wanawake watatu pekee yake kupitia njia ya simu ili aiokoe ndoa yake. Aliwafurahisha wengi aliposema kuwa aliwahi pambana na mluhya na hakujua jinsi ya kumjibu na alitumia neno moja kila wakati.

Soma baadhi ya ujumbe kutoka kwa mashabiki wa Radio Jambo waliofurahishwa na patanisho ya leo.

Susan Lulibaluliba: Wafula anapendwa na hapendeki, mwanaume Akijua unampenda zaidi Huwa anaanza madharau, anyway safi Sana, mtoto wa chips
Omar Sion: Hi patanisho imenifurahisha sana tuwao mungu awalite bat wafula asimu tharau bibi yake alimtowa akiwa km mwizi sah ni em
Rotich K K. Chebon: Very nice patanisho liked their relationship especially for njeri..white truth of love
Sammy M'arsenali: Huyo ni njeri kabisa analilia mwanaume hvyo???huyo ako tofauti.

Kindero Muthomi Benson: Mungu awabariki Kwa kazi yenu Gidi na Ghost Kwa kuleta pamoja waliotengana
Babake Humeyrah: You guyz, you have made my day tuned nikiwa hapa na toto la kimaragoli shamsa abdallah# zero37
Bae Mkali:  Hii patanisho imenifurahisha

May God bless them

Nimecheka yangu yote

Eti nakupenda sana kuliko chips, 😂🤣😂😂😂😂

Ndutaa Alisha Mwangi: The best patanisho ever, Njeri na Wafula mmenichekesha sana 🤣🤣🤣🤣
Kapweps Elisha Owuor: Patanisho ya Leo imelit up listeners (Waruu vs Salamu)
Benta Omerikwa: Patanisho ya Leo imeniongezea miaka waa nimecheka Tu sana
Perez Odhiambo: Aky njeri anapenda chipo na wafula na salamu this one has made ma day
Sheriff Kips: Mapenzi ni kuongea the two are blessed and God will continue to bless tuned from Eld
Jaysheer Wangui: Waah ya leo imeweza sana sisi wa kikuyu tukipenda huwa tunapenda na roho yote akuna kurudi nyuma,
Mc Mamba: Ain't feeling well bt nimecheka yote.that's the best ever patanisho.

Wish kupendwa ivo