Ajali Haina Kinga! Willy Paul na wachezaji wa Nandy wapata ajali

Waliosema ajali haina kinga hawakukosea.

Safari ya kuelekea Nandy Festival katika mji wa Sumbawanga, Tanzania ilikatizwa baada ya basi lake la ziara kupata ajali mapema leo hii.

Ripoti za awali zilisema kuwa wasanii wote wakuu ambao walitarajiwa  kwenye onyesho hilo walikuwa ndani ya basi hilo. Wasanii hao ni pamoja na Juma Nature Artists, Whozu, Stamina, Nandy, Barnaba, Rome, Billnass, Ice Boy na Willy Paul.

Hata hivyo, meneja wa Nandy alibainisha kuwa basi hilo lilikuwa linawasafirisha tu wachezaji na wasanii wa ziada wa wasanii wakuu.

''Basi lilikuwa limewabeba washirika wa bendi na wachezaji bali si wasanii wakuu ambao walitarajiwa jukwaani. Kwa sasa, wale ambao wamepata majeraha wamelazwa katika hospitali ya Mikumi.''

Aliongeza, ''Hakuna kifo iliyo ripotiwa kwa sasa. Safari ya kuelekea Sumbawanga kwa tamasha ya Nandy itarejelewa baadae leo asubuhi.''