'Sijui mama wa kitinda mimba wangu,'msanii wa bendi ya Gengetone Miracle Baby afichua haya

Muhtasari
  • Si mfahamu mama wa mtoto wangu wa mwisho, Miracle Baby asema
  • Niliomba na kufunga ili Mungu aweze nielekea kwa mpenzi wangu
89933082_143684070473328_4863010008041043431_n
89933082_143684070473328_4863010008041043431_n

Msanii wa bendi ya Gengetone Miracle Baby akwa kwenye mahojiano alieleza jinsi kitinda mimba wake aliachwa mlangoni mwake na mtu asiyejulikana wala kumfahamu.

Tangu siku hiyo ya kumpata mwanawe aliamua kujukumika na kumlea mwanawe

Huu hapa usimulizi wake;

 

"Nina watoto wengi lakini kuwa sahihi nina wanne,watatu ni wangu na mmoja kutwaa, niliamka na kumpata akiwa ameekwa katika besini mlangoni mwangu

Nilimchukua na nikaamua kumlea, sijui mama yake lakini kuna vile ananifanana, ako na karibu miezi saba sinauhakika alikuwa na miezi ngapi alipowachwa nyumbani kwangu." Alieleza Miracle Baby.

MIracle Baby alisema kuwa ana mchumba ilhali hawajaweza kufunga pingu za maisha naye, akieleza jinsi walivypatana msanii huyo alisema kuwa aliomba na kufunga ili Mungu aweze umuelekeza kwa mpenzi wake wa maisha