Changamoto ambazo vijana wengi hupitia endapo wamekuwa baba wangali vijana

Muhtasari
  • Changamoto ambazo wavulana wengi hupitia wakati wameanza malezi ya mapema
student
student

Makala mengi yamekuwa yakizungumzia tu mimba za mapema kwa wasichana na wala hawazingatii kuwa kuna vijana wa shule ambao bado wanaitwa baba na bado wanatarajia kuitwa baba siku za usoni wakiwa wangali vijana.

Wasichana wengi wakipata mimba au ujauzito wamekuwa wakipewa kipaumbele katika jamii zetu za sasa huku vijana wengi wakiwachwa nje.

Ndio kuna vijana wale ambao wamekuwa baba wangali vijana na wakiwa shule lakini wamepewa kipaumbele na changazmoto ambazo wanapitia kuzingatiwa?

 

Huku nikizungumza na kumuhoji mmoja ambaye amekuwa baba akiwa bado kijana alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi nilimpa msichana wa miaka 16 mimba msichana huyo alipoenda kwao alifukuzwa na kuambiwa aende kwa yule alimpa mimba

Alipokuja kwetu nami nilipewa adhabu ya kukaa na msichana huyo na kuanza maisha kutoka pale hatukuwa na chochote wala lolote

Wazazi wangu walitulipia kodi ya nyumba ya mwezi mmoja na kuniambia sasa nitafute kibarua ambacho ninaweza fanya ili tupate riziki yetu

Mama wa mtoto wangu naye hakuwa mzembe alikuwa anaenda anafanya kibarua na kisha analeta alichokuwa anapata tunajikimu nacho nami naleta yangu tuanajikimu pia

Kuwa baba ukiwa ungali kijana si jambo rahisi kama vile wengi wanavyoon, changamoto ni nyingi sana kwanza ukitafuta kazi ukiwa huna kitambullisho hapo ndipo utajua hujui

Pia unapata unatafutia tumbo tatu na wala si mbili, alafu tulikuwa tumezoea kupewa kila kitu na wazazi wetu, kuanzia maisha ndipo changamoto nyingi zipo

 

Kile naweza ambia vijana wenzangu wasikimbilie maisha wala kupenda raha sana maisha hummu nje si rahisi kama wanavyodhani wakiwa nyumbani kwa wazazi wao

Pia ningependa kuambia viongozi wakiangaia masuala ya mimba za mapema kwa wasichana pia wazingatie vijana kwa maana kunao ambao ni baba lakini hawajui la kufanya." Alizungumza Benjamin.

Huku tukiangalia katika upande wa changamoto ambazo vijana hao hukumbana nazo hizi hapa baadhi ya changamoto hizo;

1. Kuacha shule

Endapo mvulana huyo amekubali kuwa alipachika msichanna huyo kwa kuchukua majukumu sasa ataacha shule na hata kuacha masomo yake ili kushughulikia mwanawe jambo ambalo wengi bado huwa hawajalitoa kwa akili na kisha kujifanya bado wao ni watoto kwa wazazi wao huku wasifahamu majukumu ambayo yamewangoja.

2.Pesa na Kazi

Bila kazi hatapata pesa, utampata mvulana anataka pesa za haraka ili kujukumika katika mahitaji yake huku akijiuzisha na mambo yasiyostahili ili kupata pesa za haraka.

3.KUkataliwa

Kam vile mmoja wa wavulana huyo amesema ukienda kutafuta kazi unakataliwa kwa maana hajuitimu miaka ya kufanya kazi ilhali kuna majukumu ambayo yanakungoja.

Pia utawapata wengi wameanza kukejeliwa na rafiki zao huku wakiwatenga na kuwakataa, si rafiki tu hata wengi wazazi wao huwakataana kuwatumpa nje kana kwamba si watoto wao.

4.Kukubaliwa na jamii

Si wote ambao wana kibai cha kukubaliwa na jamii na watu wengi, ndio watakashifiwa kwa kitendo ambacho wamekifanya na hata wengi kutokubaliwa na jamii.

Baada ya kumkashifu mtoto haya basi kama mtoto mchukue na umueleze kinagaubaga kuwa amefanya mabaya na jinsi anastahili kuanza maisha yake kama baba mtarajiwa.

5 Kujipanga

Kwa kweli vijana wengi kujipanga huwa bado hawajipanga kwa maana wamekuwa wanaishi na wazzi wao na hwajui majukumu kama ya kuitwa baba, hapo utampata kijana amekataa kumpa msichana huyo ujauzito, kwa maana anataka maisha ya kuppewa kila wakati na hataki kamwe kujitegemea.

Swali ambalo tunapaswa kujiuliza kama wazazi je tumezungumza na watoto wetu kuhusu mimba za mapema na kutwa baba ungali kijana hasa wakati huu watoto wako nyumbani.

Wakati huu akili zao zimetulia na huenda wakafikiria mambaya na kutenda mambo yasiyostahili.

Naka kama wewe ni mvulana na umejipata atika mtego huo wa kuitwa baba kwa mapema haya basi chukua usukani na kuanza kujukumika.