UZITO WA NDOA

Ndoa Kwisha! Dadake Diamond Platnumz Esma aachana na mume wake baada ya miezi mitatu

Esma aachana na mumewe

Muhtasari
  •  Wameoana miezi mitatu iliyopita 
  •  Esma anasema mume wake huyo alikuwa akizungumza na wasichana katika instagram
  • Esma ni mama ya watoto wawili 

 

 

Esma na Msizwa ,wakati walipofunga ndoa

Dadake msanii wa Bongo  Diamond Platnumz Esma Platnumz, ametengana na mume wake   Msizwa Maulid baada ya ndoa yao kudumu kwa miezi mitatu pekee .

 Esma alitumia instagram kutoa ujumbe huo  wakati wa maswali na majibu na mashabiki wake . Esma na Msizwa walifunga ndoa julai tarehe 30 mwaka huu  na amesema alimua  kuachana naye kwa sababu amekuwa akiwatongoza wanawake wengine katika instagram yake .

 ‘VERY BAD KWA PETIT NILIZOEA SABABU WOTE TUNAJULIKANA ILA KUWA NA MTU ASIYEJULIKANA AKAJULIKANA INSTAGRAM CHANGA MOTO SABABU KUNA WAKATI ANAJISAHAU NA INSTA KULIKO MAISHA YAKE KUNA WAKATI ANAWADM WATU INSTA SOO BAD.’

Esma Platnumz, mama ya watoto wawili awali alikuwa ameolewa  na alikubali kuolewa tena na Msizwa kama mke wa tatu .

Esma

 Akieleza mbona alikubali kuolewa kama mke wa tatu ,Esma amesema alitaka kupata funzo  akiongeza ;

 ‘Ili kujua mambo mengine na kujifunza lazima ujitoe kama kafara’

  Uamuzi wake wa kuachana na mumewe ulizua maoni mbali mbali mtandaoni ;

mercy_ramsey Unatarajia kuoa lini tena Niko single Mr Msizwa.

montaner__tz Mzee wa ku dm madem 

megaoriginalest Esma kama amechoka kuvumilia. Ameona wacha isiwe taabu

 

nicelo Karma is a bitch!! That bitch slaps HARD!!!! Ya feel me!! Kwa alichowafanyia wapenzi wa kaka yake wacha aisome namba

new_carrymastory Esma alisema eti huwa unawatumia watu msg DM hii tabia haipendi eti, hivi uliona ile insta story yake ya jana nimeona tu nikupe umbea maana unaniwashaaa

shamimshaaban96 Umeachwa n Esma ndio warudi kwa melo