Tabia za kawaida ambazo zinafanana kwa wanawake ambao hudanganya katika uhusiano

Muhtasari
  • Tabia za kawaida ambazo zinafanana kwa wanawake ambao hudanganya katika uhusiano
  • Si wanaume tu pekee ambao hudanganya katika mahusiano ya kimapenzi bali hata wanawake wanatabia kama hiyo

Katika baadhi ya mahusiano ya kimapenzi si wanaume tu pekee yao ambao hudanganya katika uhusiano huo bali ata wanawake wengi hudanganya  na kumuegesha mwenzake kama gari lililoaribika.

Kuna tabia ambazo hufanana katika kila mwanamke ambaye anadanganya kwa uhusiano.

Hizi hapa baadhi ya tabia za wanawake waaina hiyo;

 

1.Hawakuangi wametulia

Kila mara wanavurugu kwa kila kitu, mara yuko hapa na pale hawatulii mahala pamoja hasa wakati anashika simu yake anataka tu kukaa pekeyake.

2.Huwa wameshikana kila mara

Hawana wakati na wenzao kila mara ana shughuli ya kufanya, ilhali si shughuli bali ana taka wakati wake na mpenzi wake wa kando.

Hata kwako kama mpenzi kila wakati atakwambia kwamba ameshikana kama unataka muende mahali au kwenye shehere.

3.Anazingatia simu yake

Macho yake yapo kwenye simu yake kila wakati ilhali umetenga muda mkae na yeye, pia utapata simu yake imeekwa namba za siri ambazo haufahamu kwa maana hataki  kitoweo kiingie mchanga.

 

4.Huwa anapeana sababu kila mara ili msifanye ngono

Katika baadhi ya mauhusiano lazima wapenzi wafanye pekejeng ili watambuane vyema lakini endapo mwanamke wako anakupa sababu mara nimo kwenye hedhi mara sihisi vyema haya basi chunguza nini shida.