Najuta sitawahi mueka mume wangu kwenye mitandao ya kijamii-Maureen Waititu ajutia haya

Muhtasari
  • Maureen Waititu akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hatawahi tambulisha mwanamume wake kwenye mitandao ya kijamii
maureen-waititu-and-frankie-696x418
maureen-waititu-and-frankie-696x418

Aliyekuwa mkewe Frankie Kiarie Maureen Waititu alifichua kuwa anajutia kuweka maisha yake hasa ya ndoa kwenye mitandao ya kijamii.

Frankie alimfanya Maureen kutimulia nyumbani mwa mama yake huku baadae wakiachana na Maureen kusema ya kwamba Frankie hawasaidii wanawe.

Drama ya wawili hao kuachana ilizungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii huku wawili hao wakiwa kwenye vichwa vya habari.

Akiwa kwenye mahojiano mama huyo alikuwa na haya ya kusema kuhusu mitandao ya kijamii;

"Tulipoanza kuwa kwenye mitandao ya kijamii tukiwa na Frankie tulikuwa wachanga sna, hatukujua chochote,hatukuwa na hatia sana, sitawahi weka ndoa yangu kwenye mitandao ya kijamii 

Naweza ambaia watu kuwa kuna mtu lakini sitawaonyesha." Alisema Maureen Waititu.

Pia maureen alisema kwamba anajuta sana kwa maana chochote ambacho kinaenda kwenye mitandao ya kijamii ni cha kudumu.

"Najuta, chochote kinachoendelea au kufanika kwenye mitandao ya kijamii ni cha kudumu, watu husemamambo ambayo hawayajui  

Ingawa ukweli unauma sitawahi onyesha au kumtambulisha mwanamume wangu kwenye mitandao ya kijamii."