Kwa nini wanawake wa Kenya wanawekeza kuliko wanaume

Kuwekeza katika maisha yako ni jambo la maana katika maisha ya kila mwanadamu,ndio kuna wale watawekeza na wale wataona hamna haja ya kuwekea kwani aijuaye kesho ni Mungu.

Kupitia kwa utafiti wanawake wakenya huwa wanawekeza sana kuliko wanaume, hivyo basi utawapata wanaume wanahangaika maishani kuliko wanawake.

Kuna wale wanaume ambao hudai kwamba wanawake hawana mahitaji mengi kama wanaume, lakini kama unataka maisha yako ya usoni husije kuteseka haya basi utapanga na kujipanga vyema.

 

Hizi hapa kwanini wanauem wa kenya hawawekezi pesa zao kama wanawake wanavyowekeza;

1.Wanume wanapenda kukopa kuliko wanawake

Utawapata wanaume watakopa pesa ili kuwapendeza wapenzi wao huku akipokea mashahara wake anarudisha mkoppo ambao alikopa.

2.Wanaume wengi hawafanyi utafiti wanapowekeza

Utampata mwanamume ameanza biashara na kwa muda mfupi inafilisika kwa sababu hakufanya utafiti kana kwamba biashara hiyo itadumu.

Lazima baadhi ya wanawake watafanya utafiti na kisha kuelewa kama biashara hiyo itawaletea faida au la ili asitupe pesa zake kichakani.

3.Wanaume wanapenda kutumia pesa zao ujivinjari

 

Ni ngumu sana kumpata mwanamke ana tumia pesa zake kujivinjari, atatumia za mwanamume lakini zake atawekeza.

Wanaume watajivinjari na wenzao na kuharibu pesa zao bila ya kujali kesho.

Je maoni yako ni yapi kuhusu wanawake kuwekeza sana kuliko wanaume?