Wewe si Mungu wacha kuhukumu watu,'Msanii Mr Seed amwambia Ringtone baada ya kumkashifu

Muhtasari
  • Mr Seed amjibu Ringtone baada ya kumkashifu kwa kutoa collabo na bendi ya Sailors
mrseedofficial
mrseedofficial

Msanii wa nyimbo za injili Mr Seed amemsjibu msanii Ringtone huku akimwambia kwamba yeye si Mungu na hapaswi kuhukumu watu hii ni baada ya Ringtone kumkashifu kwa collabo ambayo anataka kufanya na Gengetone group Sailors.

Kupitia kwenye ukurasa wake Ringtone alimuita msanii Seed kwa kufanya collabo na wanamuziki hao huku akisema kwamba anapaswa kuacha la sivyo atoke kwenye tasnia ya nyimbo za injili.

"Wachana na huu ujinga mr Seed, enda tu kwa Secular, huo wimbo wako ambao unataka kutoa na Sailors wakristo hawataupokea 

 

Bure kabisa Lubbish, MUngu hawezi kudhihakiwa." Aliandika Ringtone.

Huku Mr Seed akimjibu ujumbe wake Ringtone naye alikuwa na haya ya kumwambia,

ringtone
ringtone

“…industry ya gospel imekuwa na issues, tumekuwa na a lot of judging badala ya ku support, fighting badala ya kusupport. Mtu akitakuchnage akuwe a gospel artiste tunamjudge badala ya kumsikiza tunamjudge, which is not right. We are not God. We are not supposed to judge anyone na decision yenye amemake.

…for me ku support Lexy from Sailors venye ameamua kufanya gospel imekuwa tena shida. My friend you are not God. First of all, God did not come for the church, God alikuja kwa wale watu hawamjui, wewe unamjua ni sawa, but stop judging others, stop fighting others, it’s not right." Aliandika Mr Seed.

Haya yanajiri baada ya msanii Lexxy kutangaza kuwa anajiunga na tasnia ya nyimbo za injili huku akiwaaga waimbaji wenzake.