Tazama picha za Kanze Dena zilizozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii

Muhtasari
  • Kanze Dena azua mjadala kwenye mitandao baada ya kuongeza uzito wake

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena Ijumaa Januari 29 alizua mjadala kwenye mtandao baada ya kuonekana kuongeza uzito pakubwa.

Wanamtandao hawakukosa kutambua kubadilika kwa Kanze na mara moja waliingia kwenye kurasa zao kuelezea walichokiona.

Baadhi yao walisema unene wake ni kutoka an kujifungua hivi karibuni na hivyo basi athari za ujauzito bado hazijamtoka. 

Kabla ya kujiunga na Ikulu, Kanze alikuwa mmoja wa mwanahabari tajika wa runinga ya Citizen ambapo alisoma taarifa pamoja na Lulu Hassan.

Mjadala uliibuka baada ya msemaji huyo kuhotubia wanahabari baada ya rais Uhuru Kenyatta kuwasili Sagana kaunti ya nyeri kwa ziara yake ya siku 4.

Hizi hapa baadhi ya picha zake Kanze Dena;