DJ Evolve husema kwamba Babu Owino alikuwa rafiki yake-Baba Evolve afunguka

Muhtasari
  • John Orinda asema Babu Owino alikuwa rafikiye Evolve
  • Pia alisema kwamba alimshukuru Babu kwa kumpeleka mwanawe hospitali kwa wakati ufaao

Baba yake mcheza santuri DJ Evolve akiwa kwenye mahojiano na radiojambo aliweka mambo bayana kuhusu maisha ya mwanawe na jinsi ajali ilivyotendeka.

Baba Evolve alisema kwamba mwanawe alisema kwamba Babu Owino alikuwa rafiki yake.

"KIjana wangu alisema kwamba Babu alikuwa rafiki yake,ata marafiki wenzake walipokuja alisema maneno hayo

jinsi ajali hiyo ilivyotokea hamna mtu ambaye anajua kwa maana hawakugombana wala kuzua vurugu, Felix alishtukia ameanguka hakujua kwamba ni yeye amepigwa risasi

Babu Owino alimpeleka hospitali kwa wakati ufaao, na madaktari walianya kazi nzuri sana," Alisema Orinda.

Orinda pia alisema kwamba huwa hawazungumzi na Babu, ilhali huwa wanazungumza naye kupitia madaktari ambao wanamtibu DJ Evolve.

Kuna wakati ambao Orinda alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumshhukuru Babu Owino kwa kumpeleka Evolve Hospitali.

"Nilikejeliwa kwa kumshukuru Babu, lakini aliokoa maisha ya mtoto wangu, kwa kumpeleka hospitali wakati ufaao hiyo ndio maana nilisema asante

Mtoto wangu angeaga dunia wakati huo sijui nini ingefanyika wakati huo,na ningekuwa wapi, lakini kwa hayo yote namshukuru Mungu kwa maana mtoto wangu yuko hai,"