Mume wangu aliniambia kuwa amepata size 8 hanihitaji-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi mumewe alimuacha baada ya kumpa majeraha
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Wanawake wengi wamekuwa wakipitia dhuluma na mateso katika ndoa zao huku wengine wakiachawa na majeraha katika miili zao.

Baadhi ya wanawake hao wamepasa sauti zao na kuanza kutetea haki za wanawake huku wengine wakiumia kisiri.

Mwanamke mmoja alisimulia jinsi mumewe alimchapa na kumwambia kwamba amempata mwanamke mwenye umbo nzuri ambaye sio mnenen kama yeye.

 
 

"Nimekuwa kwa ndoa kwa miaka 5,nilimuachia mume wangu watoto kwa maana miaka hiyo yote amekuwa na kiburi na hata kuniambia kwamba hanipendi

nilisikia nimechoka wakati aliniambia kwamba amempata mwanamke amabaye ana umbo ya size 8, kabla ya kutoka kwenye ndoa yangu alinipa kichapo cha mbwa mpaka nina majeraha kwenye uso wangu ambayo aliniweka

Kwa kawaida mwanamke ni uso lakini aliharibu uso wangu, sasa anataka turudiane jambo ambalo siwezi dhubutu," Alisimulia mwanamke.

Je ni jambo lipi ambalo lilifanya utoke kwenye ndoa yako au uhusiano wako?