'Sitawahi pakia mpenzi wangu kwenye mitandao ya kijamii tena,'Muigizaji Joyce Maina asema

Muhtasari
  • Joyce maina asema hatawahi pakia mpenzi wake mitandaoni
  • Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miezi chache

Muigizaji wa kipindi cha Monicah na mtangazaji Joyce Maina, amesema wazi kwamba hatawahi pakia mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Usemi wake unajiri siku chache baada ya kuweka wazi kwenye mitandao ya instagram kwamba waliachana na mpenzi wake mtangazaji Tony Kwalanda.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miezi chache.

 

Huku akiwa kwenye kipndi chao alikuwa na haya ya kusema,

"Nilikuwa na pakia mpenzi wangu wangu kwenye mitandao ya kijamii lakini sitawahi fanya hivyo tena

Tony Kwalanda ana picha zetu kwenye mitandao ya kijamii, na sijui kwa nini nimekuwa kwenye hii tasnia kwa miaka kumi na watu hawajawahi jali kuhusu Joyce Maina na sijui kwanini sasa wanataka kujua,"Aliongea  Joyce Maina.