'Kujiua sio suluhisho,'Akothee amwambia shabiki aliyetaka msaada

Muhtasari
  • Wakati huu wa sasa wananchi wengi wanapitia magumu na changamoto nyingi, wakati nchi inakabiliana na janga la corona
  • Akothee amshauri shabiki aliyetaka kujiua

Wakati huu wa sasa wananchi wengi wanapitia magumu na changamoto nyingi, wakati nchi inakabiliana na janga la corona.

Kuna baadhi ya watu ambao wamepoteza kazi zao, na hata biashara kudhoofika, baadhi ya watu wameomba msaada kutoka kwa wasanii tofauti.

Msanii Akothee alipakia ujumbe wa mwanamke mmoja ambaye alitishia kujiua kwa sababu ya changamoto ambazo anapitia.

 

Akothee alimshauri na kumwambia kwamba kujiua sio suluhisho la shida zake, huku akiomba mashabiki wamsaidie.

"Kujiua sio suluhisho mpendwa, utawaachia watoto nani, msaidieni Lilian na kile chochote uko nacho alipe kodi ya nyumba na pia kununua chakula," Aliandika msanii huyo.

Kwa muda sasa Akothee amekuwa akiwasaidia wananchi wanyonge na wale ambao wamekuwa wakimuomba msaada.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki, huku wengi wakimshauri Akothee kwamba anaweza kumsaidia pekeyake;

gloriah__gich: Madam boss funga macho tu we believe in u.

hildah.montez: Madam boss you can do that alone

chef.hellen: Madam you can do that without us.nakutambua cheza Kama weee

phylislukuyu: Ata wengine tukiamua kukuinbox c inbox yako itabiga nduru

oramisimoses: @akotheekenya hata kama sina chakutoa napongeza kazi yako nzuri be blessed always