'Nakupeza sana,'Anerlisa Muigai amuomboleza dada yake Tecra mwaka mmoja baada a kifo chake

Muhtasari
  • Anerlisa Muigai amuomboleza dada yake Tecra mwaka mmoja baada a kifo chake
  • Huku wakimkumbuka familia yake ilitengeneza picha nyumbani mwao ili kumuomboleza mwendazake Tecra
Tecra
Tecra

Mwaka jana siku kama hii Familia ya Anerlisa Muigai walimpoteza mpendwa wao Tecra Muigai baada ya madai alianguka kutoka kwa ngazi nyumbani alimokuwa anaishi.

Huku wakimkumbuka familia yake ilitengeneza picha nyumbani mwao ili kumuomboleza mwendazake Tecra.

Kulingana na familia wanaamini kwamba Tecra aliuawa na wala hakuanguka kutoka kwa ngazi.

 

Kupitia kwa video ambayo Anerlisa alipakia kwenye ukurasa wake wa instagrama alinionekana akiwa anaomba kabla ya kuweka maua kwenye picha ya dada yake.

Anerlisa aliandika ujumbe huu;

"Mwaka jana siku kama hii ya leo,dada yangu alupimua pumzi yake ya mwisho,tafadhali wacha tumtumie Tecra nguvu nzuri, endelea kupumzika kwa amani dada yangu mpendwa

Nakupeza tena sana," Aliandika.