TBT:Mashabiki wapendezwa na picha ya zamani ya muigizaji Sandra Dacha

Muhtasari
  • Mashabiki wapendezwa na picha ya zamani ya muigizaji Sandra Dacha
  • Sandra alofahamika sana kupitia uigizaji wake katika kipindi cha 'Auntie Boss' kilichokuwa kinapeperushwa katika runinga ya NTV
Screenshot-from-2020-06-09-08_34_25
Screenshot-from-2020-06-09-08_34_25

Muigizaji Sandra Dacha almaarufu Silprosa ni mmoja wa waigizaji nchini ambao wamejipenda jinsi walivyo na wala hawajali kejeli kutoka kwa mashabiki.

Sandra alofahamika sana kupitia uigizaji wake katika kipindi cha 'Auntie Boss' kilichokuwa kinapeperushwa katika runinga ya NTV.

Wengi wanafahamu hadithi yake Sandra jinsi alivyowapoteza wazazi wake wakiwa na umri wa chini huku akipitia changamoto nyingi kama mtoto wa kike.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram kipusa huyo alipakia picha yake ya zamani, huku mashabiki wakipendezwa na picha hiyo.

Baada ya kupakia picha hiyo aliandika ujumbe na kueleza jinsi mpenzi wa wakati huo alikuwa anampenda na hangeishi bila yeye.

"Tutazungumzia viatu baadaye, sio viatu bya kawaida zilini gharimu Sasa hapa boychild alikuwa ameniita date Moto Sana pale town. Sema kupiga LOOK! Boychild couldn't live without me bana! Lakini sasa Evans wewe uliniwacha ukaenda wapi aki na vile hukuwahi pumua bila mimiπŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚ Somebody please tag Evans for me πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚," Aiandika Sandra.

Haya hapa maoni ya mashabiki;

aggie_the_dance_queen: Evans tunakutafuta prissπŸ˜‚πŸ˜‚

wayua.wayua: Hizi viatu kukiwa na jua mguu inageuka nyam chomπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

kemuntobarongo: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚kumbe si mimi tu nilivaa hizo viatu

tesmuriuki1: hahaha izo viatu karibu mtu azioshe pamoja na vyombo,hehe plastic kanyagaπŸ˜‚πŸ˜‚

harry_uhuruIt's:  the handbag for meπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚