Mtangazaji Massawe Japanni amtetea mwanahabari wa KTN Sophia

Muhtasari
  • Mtangazaji Massawe Japanni amtetea mwanahabari wa KTN Sophia
Massawe Japanni
Image: Studio

Mitandao ya twitter Alhamisi iliwaka moto huku baadhi ya wanamitandao wakidai kwamba wanamtaka mtangazaji wa zamani wa runinga ya Citizen Hussein Mohammed kurejea kazini.

Hii ni baada ya mtangazaji wa runinga ya KTN Sophia Wanuna, kumuhoji naibu rais William Ruto usiku wa Alhamisi, na baadhi ya wanamitandao kudai hakufanya kazi yake vyema na kuanza kumkejeli.

Kuna wale pia walimtete Sophia na kusema kwamba alifanya kazi yake vyema.

Sekta ya wakenya walidai kwamba Mohammed ndiye alijua vyema jinsi ya kuwahoji wanasiasa, na jinsi ya kuwauliza maswali.

Hii ni baada ya Ruto kukwepa maswali alilokuwa akiulizwa na mwanahabari Sophia Wanuna.

Siku ya Ijumaa, katika kitengo cha bustani la Massawe, mtangazaji huyo alimtetea Sophia na kudai kwamba alifanya kazi nzuri na kwamba anamtetea mwanahabari mwenzake.

Massawe alisikitishwa na jinsi wanawake wamekuwa katika mstari wa mbele kukejeli wanawake wenzao.

"Mwana habari Sophia alifanya kazi yake vyema, wakati wa mahojiano, inauma sana kuona wanawake ndio wako katika mstari wa mbele kumkejeli mwanamke mwenzao," Massawe alinena.