'Wababa wengi sana wanapenda ikiwa hivi,'Muigizaji Silprosa kwa wanaume wanaomkejeli kwa ajili ya mwili wake

Muhtasari
  • Muigizaji Silprosa awatumia ujumbe wanaume wanaowakejeli wanawake wenye mwili mkubwa
Screenshot-from-2020-06-09-08_34_25
Screenshot-from-2020-06-09-08_34_25

Kwa muda mrefu sasa,  wanawake wenye mwili mkubwa kuwamekuwa wakipokea unyanyapaa na kejeli kila wakati. Walakini, sio wote wanaotikiswa na njia ya watu kuzungumza.

Wengine wana ujasiri wa kutosha na wanapenda jinsi wanavyoonekana.

Kwao, kuwa na ukubwa wa kawaida haimaanishi kuwa wao ni chini ya wanawake ambao wwana umbo nzuri na wembamba.

Muigizaji Sandra Dacha maarufu Silprosa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwaonya wanaume ambao wanatabia ya kuwakejeli wanawake wenye mwili mkubwa.

Alifichua kwamba anapata wanaume wengi wanaompenda lakini wengi wao huja na hali moja ya kudhalilisha. Kwamba lazima kwanza apoteze uzito ili wamkubali kama mpenzi wake.

"Wapenzi wanaume,Ikiwa una doa laini kwa wanawake wembamba, nenda kwao. ... lakini usije kwangu kuniambia unanitaka lakini ili niwe nawe, ninahitaji kupunguza uzito. Oya! Kwani kuna neema unanifanyia?

Nenda tu na utongoze aina yako! Hii nyama kuna wababa wengi sana wanapenda ikiwa hivišŸ¤£šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ¤£," Aliandika Silprosa.