'Naumwa!' Mtangazaji Linda Oguttu asimulia anayoyapita baada ya kupatikana na COVID-19

Mtangazaji huyo amesema kuwa amepoteza hisia ya harufu na ladha

Muhtasari

•Mtangazaji huyo amesema kuwa amekuwa akisumbuliwa na homa kali.

•Oguttu amehimiza Wakenya wote waendelee kuvaa barakoa na kusafisha mikono

Image: HISANI

Mtangazaji wa habari  mashuhuri Lindah Oguttu ametangaza kuwa amepimwa na kupatikana na virusi vya Corona.

Akitoa tangazo hilo kupitia mtandao wa Twitter, Oguttu amesema kuwa amekuwa akisumbuliwa na homa kali.

Mtangazaji huyo amesema kuwa amepoteza hisia ya harufu na ladha.

"Nimepimwa na kupatikana na virusi vya Corona na wacha niwaambie, ile homa inakuja na maradhi haya ni mbaya. Harufu hakuna! Tilapia kutoka Yurop inaonja kama sponji(Mwiko). Mwili yote inauma. Tumeni Kaluma,Rob, supu n.k. Naumia," Alisema Oguttu.

Oguttu amehimiza Wakenya wote waendelee kuvaa barakoa na kusafisha mikono.

Wanamitandao wameendelea kumtakia afueni ya haraka mtangazaji huyo.