Nilimtazama mpenzi wangu akienda na mwanamume mwingine baada ya kuhitimu chuo kikuu-Jamaa asimulia

Muhtasari
  • Je umewahi jitolea na kumlipia mpenzi wako ada ya shule, katika chuo kikuu na mambo yakabadilika baada ya kuhitimu?
  • Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitolea na kuwasomesha wapenzi wao, bila ya kujali kesho yao
sad man
sad man

Je umewahi jitolea na kumlipia mpenzi wako ada ya shule, katika chuo kikuu na mambo yakabadilika baada ya kuhitimu?

Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitolea na kuwasomesha wapenzi wao, bila ya kujali kesho yao.

Ndio kuna wale akihitimu masomo yake ya chuo kikuu, hukaa pamoja na kupendana na kuanzisha familia ilhali kuna wale huwatema wenzi wao baada ya hayo yote.

Nikiwa katika ziara yangu Jamaa mmoja alieleza jinsi alimtazama mpenzi wake akienda na mwanamume mwingine baada ya kuhitimu chuo kikuu.

Huu hapa usimulizi wake

"Nilipatana na mpenzi wangu baada yake kumaliza kidato cha nne, nilimuahidi kwamba nitamsomesha hadi haitimu masomo yake ya chuo kikuu

Nililipa ada yake, na hata kumpa pesa ya matumizi, baada ya miaka nane nikiwa namgonja, hakunialika katika hafla ya 'graduation' nilienda lakini nilimpata na mwanamume mwingine ambaye alikuwa ananiamia ni binamu yake

Nilipomuuliza aliniamba kwamba mimi sio wa kiwango chake, niliwatazama wakienda kuingia kwa gari la mwanamume huyo," Alieleza Jamaa huyo.