'Hakuna ushauri wa bure,'Akothee asema itamgharimu mtu laki 100 kumpa ushauri

Muhtasari
  • Akothee asema itamgharimu mtu laki 100 kumpa ushauri
Akothee
Image: hisani

Msanii Akothee sio mgeni kwenye mitandao ya kijamii, anafahamika sana hasa kupitia kwa kazi yake ya usanii.

Ukimzungumzia msanii huyo wengi wanamfahamu kwa uamuzi wake wa maisha na kwa jina la 'President of single mothers' kama anavyojiita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesema kwamba itamgharimu mtu laki 100 ili ampe ushauri.

Pia alisema kuwa muda ni pesa, na hamna ushauri wa bure.

"Haloo Akothee nataka kuzungumza nawe.BINAFSI! OYAA 100K

Hakuna ushauri wa bure zaidi, wakati ni pesa kwangu, kwa hivyo nachaji 100,000 kwa kila kikao. Kalenda yangu ya 2021 imeshikana sana."

Ni ujumbe ambao ulipokelewa na mashabiki kwa hisia tofauti na hizi hapa hisia zao;

mwallow_arts_ke: Ooh pekee..pesa otas am coming soon with an art chokee😂

_r.o.y_taylla: Waaah pesa otas madam boss kumbe😢

caynan_b.r.a.g.a.n: Madam president unaenda Kibarua na stick on😂😂 like what iss!!!???😂😂

sting_wela_wela: Take 65000 please ama uache

joyblessed9998: Wengi wakukuona ni shida zinawaleta kuomba msaada mamaa watatoa wapi na wamelala njaa yawa😢😢😢