Nampenda kama hanipendi hiyo ni shauri yake-Akothee asema haya kuhusu mpenzi wake

Muhtasari
  • Ni dhahiri kuwa mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu kama Akothee na aliyekuwa meneja wake Nelly Oaks wanachumbiana
Akothee na Nelly Oaks
Akothee na Nelly Oaks
Image: INSTAGRAM

Ni dhahiri kuwa mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu kama Akothee na aliyekuwa meneja wake Nelly Oaks wanachumbiana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amedai kuwa anampenda Oaks na kama hampendi hiyo ni shauri yake kwani hamna aliye na roho yake.

Ujumbe wake Akothee ulionekana kuwaendea wanamitandao wale wamekuwa wakikosoa uhusiano wake na mpenzi wake.

"Unajua nasema Ninachohisi na jinsi anavyonifanya nijisikie. Ninampenda, ikiwa hanipendi tena

hiyo ni shauri yake isikuume ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚, kwani una roho yangu ? ,Mimi Niko na mpenzi wangu , ndani ya mapenzi ,tunakunywa @orchidvalley_ke .hamna mwanamume anayefanya nihisi ninavyohisi sasa.Baby utakunywa mango ama guava ? ๐Ÿ’‹," Akothee aliandika.

Mama huyo wa watoto 5 anafahamika sana kwa bidii yake katika kazi yake ya usanii na biashara.

Baada ya kumtambulisha mpenz wakke mitandaoni wengi walijawa na hisia tofauti, lakini hayo hayakumfanya Akothee arudi na nyuma au kuacha kipenzi chake.