Watoto wakiachwa na baba waambie alikataa kuwalea-Loise Kim awashauri wanawake

Muhtasari
  • Msanii wanimbo za injili za kikuyu Loise KIm kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekuwa akiwashauri akina mama

Msanii wanimbo za injili za kikuyu Loise KIm kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekuwa akiwashauri akina mama.

Sio akina mama tu haswa wale wameachwa na waume wao na kuwaachia watoto wateseke.

Katika karne hii ya sasa  wanawake wengi wanawalea watoto pekeyao, baada ya baadhi ya wanaume kukataa kujukumikia mahitaji ya watoto wao.

Pia alisema kwamba akkina mama hawapaswi kuwadanganya watoto wao kwamba baba yao alikanyangwa na lori, bali waambie ukweli kwamba baba yao alikataa kuwalea.

"Watoto wakiachwa na mababa zao, tell them the truth. Wacha kuwaambia ati alikanyangwa na Lori. Mwambie, alikataa kukulea, nikaamua kucheza kama mimi.Lazima nikulee," Aliandika Loise

Hizi hapa hisia za wanamitandao, walizozitoa baada ya ujumbe wake msanii huyo;

paulineshiks: πŸ‘πŸ‘ Ukweli wa mambo

sylviachemjor2: Ongeza volumeπŸ”₯πŸ”₯

njeriwambui032: Volume iko juu sana❀❀❀

shikky_shixIyo: volume iko sawa mami

winniegathura: Great words from Anne Murathe πŸ‘

flo.mash: Ushasema πŸ™ŒπŸ™Œ