'Wacheni tu ufala na mfanye ile kazi mliitisha,'Mchekeshaji Jaymo Ule msee awasuta Uhuru na Ruto

Muhtasari
  • Mchekeshaji Jaymo Ule msee awasuta Uhuru na Ruto
  • Pia mchekeshaji huyo aliwakumbusha kwa aliwapigia debe, walipokuwa wanataka kuwa viongozi wa kenya
Image: Instagram/Jaymo ule msee

Mchekeshaji Jaymo Ule msee kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewataka rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto watatue shida zao kama watu wazima.

Pia mchekeshaji huyo aliwakumbusha kwa aliwapigia debe, walipokuwa wanataka kuwa viongozi wa kenya.

Aidha aliwakumbusha vigogo hao wawili kwamba waliahidi kufanya kazi na wala sio kupigana hadharani.

" Kwa Rais Uhuru na Naibu Rais Ruto, mimi ni Mkenya niliyewapigia kampeni na nikawapa kura yangu nikijua mtatuongoza, tafadhali wacheni hizi sarakasi zote ambazo mnatuonyesha hadharani na mfanye kazi.

Mlituambia kwamba tuwapigie kura ili mbadilishe maisha yetu, kama mna tofauti, tatueni kama watu wazima ama muache kutuonyesha hadharani, mnaleta migawanyiko mingi miongoni mwa vijana wengi ambao walirauka kuwapigia kura," Alisema Jaymo. 

Pia aliwaambia kwamba endapo vita vitatokea mwaka ujao, wao ndio watakuwa kini kikubwa cha kusababisha mapigano.

" Wachana na haya mambo ya kijinga na mfanye kazi ambayo mliomba na mkapewa. Vijana wakipigana mwaka wa 2022, kumbuka bado nyinyi ni wateja kule ICC," Aliongezea Jaymo. 

KItumbua kiliingia mchanga katika uhusiano wa Rais Kenyatta na naibu wake Ruto,baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017

Vigogo hao wawili wamekuwa wakitupiana vijembe hadharani.