Mpenzi wangu alikuwa ananilipia kodi ya nyumba nilipokuwa sina pesa-Omanyala afichua haya

Muhtasari
  • Mwanariadha Omanyala afunguka kuhusu maisha yake
  • Wakati wa hafla ya ODI ambayo ilikuwa inapeperushwa  kwenye runinga ya NTV, Ferdinand Omanyala amefunguka kuhusu mke wake Lavender Omanyala
Omanyala na mkewe
Image: Hisani

Ferdinand Omurwa Omanyala anaweza kuwa ndiye mwanaume mwenye kasi zaidi barani Afrika baada ya kuvunja rekodi ya bara la Afrika katika mbio za mita 100.

Alikimbia kwa kasi ya sekunde 9.77 katika mbio za Kip Keino Classic mjini Nairobi na kuvunja rekodi ya sekunde 9.85 iliyowekwa na raia wa Afrika Kusini Akani Simbine mwezi Julai.

Wakati wa hafla ya ODI ambayo ilikuwa inapeperushwa  kwenye runinga ya NTV, Ferdinand Omanyala amefunguka kuhusu mke wake Lavender Omanyala.

Kulingana na Omanyala mkewe ndiye alikuwa anamlipia kodi ya nyumbani alipokuwa hana pesa.

Pia alisema kwamba wakati umefika wa kumtunza mkewe, kwani amekuwa akishika moko katika safarii yake.

Wakati wa tukio ambalo lilifanyika kufahamu bingwa, Ferdinand Omanyala alifichua zaidi kwamba mkewe alikuwa akimkanda baada ya mazoezi yake ili misuli yake iwe sawa.

"Milifanya mazoezi kwa miezi 6 bila ushandani wowote, na hatukuwa na pesa, nilikuwa najifunza bila malengo yoyote

Haya yote nashukuru mpenzi wangu, kwa kunitunza amekuwa katika safari hii yangu, alikuwa analipa kodi ya nyumba na kutunza bili zingine wakati huo sikuwa na pesa

Sasa ni wakati wangu wa kuhakikisha nimemtunza na kumpa kila kitu anachotaka," Omanyala alizungumza.

Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja  Odi Bets ilimshukuru Lavender kwa gari kwa ajili ya kumwamini mumewe na kusimama naye.

 Baba yake pia alipewa hundi ya kumthamini yeye kwa kusimama na mwanawe.