'Nitapumzika kwa kaburi,'Mwanasosholaiti AmberRay amjibu shabiki

Muhtasari
  • Hata hivyo ameeleza kwamba hakuna ugomvi wowote kati yake na mfanyibiashara huyo mashuhuri aliyekuwa amemuoa kama mke wa pili
  • Amber Ray alipoulizwa kwa sasa anachumbia nani alidai kwamba anajichumbia mwenyewe
Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii, kwa kweli unamjua na kumfahamu mwanasosholaiti Amber Ray.

Mwanasosholaiti huyo amekuwa akivuma kwa muda sasa baada ya kufichua uhusiano wake na mfanyibiashara Jamal Roho Safi, lakini waliachana.

Katika kipindi cha maswali kwenye motandao ya kijamii ya instagram, Amber aliweka wazi kwamba yuko 'songle' na kwa sasa hataafuti mwanamume au mpenzi.

Kupitia kwenye kipindi hicho mmoja wa mashabiki wake alimshauri akapumzike na awache raha.

"Wacha raha sasa dada kaa upumzike," Shabiki alimwambia.

"Nitapumzika kwa kaburi," Amber Alimjibu.

Takriban miezi miwili baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake mfanyibiashara Jimal Rohosafi, Ray ameweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba na kusisitiza kuwa hayuko katika harakati za kutafuta mwenza.

"Niko single na wala sitafuti" Alisema Ray.

Hata hivyo ameeleza kwamba hakuna ugomvi wowote kati yake na mfanyibiashara huyo mashuhuri aliyekuwa amemuoa kama mke wa pili.

Amber Ray alipoulizwa kwa sasa anachumbia nani alidai kwamba anajichumbia mwenyewe.

Ray pia alipuuzilia mbali uvumi uliodai kwamba wako kwenye uhusiano wa mapenzi na mchekeshaji Eric Omondi.

Hivi karibuni uvumi kuwa wawili hao huenda wameamua kujitosa kwenye mahusiano ulienezwa mitandaoni baada yao kuwasiliana hewani kwenye mtandao wa Instagram huku wakiitana majina matamu ya mapenzi.