Pesa Otas!Diamond Platnumz anunua saa ya milioni 3.3

Muhtasari
  • Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Olatnumz, ni mmoja wa wasanii ambao wanajua kutumia pesa kujiburudisha
  • Saa mpya ni nyongeza tu ya mkusanyiko wa saa za gharama kubwa za Chibu Dangote
Diamond Platnumz
Image: Instagram/Diamond

Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Olatnumz, ni mmoja wa wasanii ambao wanajua kutumia pesa kujiburudisha.

Platnumz ambaye kwa sasa yuko ziarani nchini Marekani, alishiriki risiti za matumizi yake ya hivi karibuni kupitia hadithi zake za Instagram.

"Milioni 69 kwa Saa" Aliandika Diamond Platnumz.

Saa mpya ni nyongeza tu ya mkusanyiko wa saa za gharama kubwa za Chibu Dangote.

Agosti mwaka huu Diamond aligonga vichwa vya habari baada ya kununu mkufu ulioandikwa jina lake uliogharimu milioni 5.2.

Pia msanii huyo alifichua kuwa mkufu huo ulimgharimu USD 48,000, huku ikilinganishwa na pesa taslimu za kenya ikiwa ni milioni 5,238,595.20.

Aliwashauri vijana waache kuvalia mikufu bandia kwani kuna saratani.

" Dhahabu na Almasi💎 #HalfManHalfLion acheni kuvaa mkufu bandia wavulana wadogo ... kuna saratani ✌🏼....USD 48,000…Tsh! 111,360,000 Aye ye ye! Naondokaje sasa???kwanza nawahi nini wakati nimeachwa????" Aliandika Diamond.