'Ndoto yetu imetimizwa,'Victor Wanyama amsifia mwanawe na muigizaji Serah Teshna

Muhtasari
  • Victor Wanyama amsifia mwanawe na muigizaji Serah Teshna
Image: Hisani

Baada ya muigizaji Serah Teshna kutangaza kuwa wamebarikiwa na kifungua mimba siku 40 zilizopita, wanamitandao marafiki na mashabiki walimpongeza kwa baraka tele.

Kulingana na Serah Mungu amekuwa mwema mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa mwanakandanda Victor Wanyama,amemlimbikizia sifa Serah Teshna na mtoto wao sifa.

Wanyama amesema na kukiri kwamba ndoto yao ambayo wamekuwa wakiisubiria kwa muda imetimizwa.

"Tumefurahia @serahteshna Ndoto yetu ya muda mrefu sana ya uzazi hatimaye imetimizwa na kuwasili kwa mkuu wetu mdogo wa thamani. Mungu ni mzuri. Asante nyote kwa upendo na msaada tunashukuru," Aliandika Wanyama.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki;

loulou_hassan:Hongera Shem πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½

jalangoo: Congratulations King!

wanjikustephens: Congratulations are inorder champπŸ™Œ

honalinur: Congratulations brother

Serah alijibu ujumbe wa mpenzi wake na kusema kuwa;

"Hatimaye tunaye binadamu mdogo nusu mimi na nusu wewe, baraka tele."