'Nililazimishwa kuolewa,'Manzi wa Kibera baada ya kuachana na mume wake

Muhtasari
  • Manzi wa KIbera adai alilazimishwa kufunga ndoa
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Image: Instagram

Huenda ndoa kati ya mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera na mcheshi Obidan Dela imegonga mwamba takriban wiki mbili baada yao kufunga pingu za maisha.

Matendo ya wanandoa hao wawili ya hivi karibuni kwenye mtandao wa Instagram yameashiria wazi kwamba huenda tayari kitumbua kimeingia mchanga.

Siku ya Jumanne mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Kibra alipakia video iliyoonyesha moyo ambao umevunjika mara mbili na kuiambatanisha na emoji za kilio.

Kulingana na wanamitandao na mashabiki wake mwanasoshalaiti huyo anatafuta kiki na wala haikuwa ndoa halali.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Manze wa Kibera, alidai kwamba alilazimishwa kuolewa, licha yake kukataa harusi hiyo.

Alifichua haya huku akiwapa wanandoa wachanga, kutofanya maamuzi kutokana na shinikizo.

"Ushauri wangu kwa wanandoa wachanga msiwahi kukimbilia katika mambo kama vile kufanya harusi au kupata watoto kwa sababu ya shinikizo. Nililazimika kufanya hivi ingawa niliendelea kusema tupeanae  wakati."

Manzi wa Kibera aliendelea kueleza kuwa hawezi endelea kuvumilia tena kwani kwa muda sasa hajakuwa na raha.

"Siwezi shikilia zaidi.. sijakuwa na furaha" Manzi wa Kibera aliandika.

Je hii ni kiki au ni jambo la kweli, unaweza kutoa maoni yako kwa ushuri zaidi.