Tushaazoea kiki,'Wanamitandao wamwambia Caro Sonie baada ya kudai wametangana na Mulamwah

Muhtasari
  • Wanamitandao watoa hisia tofauti baada ya Caro kuthibitisha kutengana na Mulamwah
Mulamwah na Caro Sonie
Image: INSTAGRAM/CARO

Baada ya baby mama wa mchekeshaji Muamwah,Caro kutangaza kutengana kwao mashabiki wametoa hisia tofauti, huku baadhi yao wakisema kwamba wanatafuta kiki.

Carol Sonnie ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kutengana kwao.

Ingawa hajafichua sababu za kutengana kwao, Muthoni amesema walifanya makubaliano ya pamoja huku akimshukuru baba ya binti wake kwa kipindi cha miaka minne ambacho wamekuwa pamoja.

"Hii ni kuweka wazi kuwa mimi na Mulamwah hatuko pamoja tena. Sote tumekubaliana na kuamua kuachana kwa sababu zinazojulikana kwetu. Asante sana kwa upendo na usaidizi mliotupa kwa miaka hiyo 4, mimi binafsi sichukulii kawaida.

Kwa mulamwah, Asante sana kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako kwa miaka hiyo.  Nashukuru sana na nitahifadhi kumbukumbu milele. Katika hatua yako inayofuata maishani, sikutakii kingine ila bora.Endelea kushinda na Mungu akubarikikatika  kila hatua ya maisha yako" Muthoni ameandika.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

dramah_doll: Clout ,,tumezoea😢😢

amsashamalkia: Mara ya pili 🤣🤣aiiii kamum jaribu mwingine aki

munyonge_jr: Wagikuyu jameni.. Ndio uitishe upkeep ukitumia mtoto🤣

jaci__nta: No no no no no my gal..oooiii haki...but ka umeamua nisawa tu..I wish it wasn't this way..God direct uu gal..much love❤️❤️❤️

lavmoh_culture: Alafu mtu ananiambia nioe, acha tukulane tu na tuzalishe😂

nyar_otis: Mta clout chase mpaka it will come to reality…rem the power of

deniqueavril: Waaah yaani ulingoja tu ujifunguwe ndio utubebee mtoto😢sawa tu but sisi kama waluhya chetu huwa hakiendi wala hakipotei anyway mbele kuzuri