Huwezi furahia ngono na kukimbia majukumu-Robert Burale awaonya 'dead beat dads'

Muhtasari
  • Wanamitandao mitandaoni walikubaliana na kauli ya Burale huku baadhi yao wakimkejeli, kwa ajili ya kauli yake
Robert Burale
Robert Burale

Mtangazaji wa hafla, mtaalamu wa mikakati ya uuzaji na mwigizaji, Robert Burale, amezua hisia tofauti mtandaoni baada ya kauli yake ya kuwaonya akina baba ambao hawajukumikii mahitaji ya watoto wao, kusambaa mitandaoni.

Wanamitandao mitandaoni walikubaliana na kauli ya Burale huku baadhi yao wakimkejeli, kwa ajili ya kauli yake.

Kauli ya Robert Burale kwa vijana ni kwamba wanapaswa kujitokeza na kutekeleza majukumu yaliyoambatana na matendo yao.

Robert Burale alisema kuwa ikiwa hauko tayari kuwa baba au kutunza mtoto, hupaswi kamwe kulala na mwanamke yeyote lakini badala yake funga zipu ya suruali yako na ujiepushe, mpaka siku utakapokuwa umekomaa vya kutosha na kuyasimamia majukumu yaliyotokana na matendo yako.

Aliwakanyaga wale wanaume wanaowapa wanawake mimba na kukimbia majukumu ya kulea mtoto.

Kulingana na Burale, hupaswi kufurahia ngono na kukimbia majukumu.

"Kama huyuko tayari kujukumikia mahitaji ya mtoto wako, haujakomaa vya kutosha kufungua zipu ya suruali yako

Ni jambo la kusikitsha sana kumpa mwanamke ujauzito, na anapokwambia ana ujauzito unatoroka ka sababu hakuavya mimba yako, sikizeni wanaume huwezi furaia ngono na kukimbia majukumu," Alizungumza Burale.