Dem akikuita kwake jua hakupendi,'Samidoh awashauri wanaume msimu huu wa Valentines

Muhtasari
  • Samidoh awashauri wanaume msimu huu wa Valentines
  • Imesalia siku 6 tu, ili siku ya wapendanao ifike, huku wengi wa wapenzi wakisuburia kuonyeshwa mahaba tee na wenzi wao

Msanii wa nyimbo za Mugithi Samidoh Muchoki, kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram amewashauri wanaume jinsi ya kujichunga wakati wa siku ya wapendanao.

Imesalia siku 6 tu, ili siku ya wapendanao ifike, huku wengi wa wapenzi wakisuburia kuonyeshwa mahaba tee na wenzi wao.

Ni siku ambayo hushserehekewa kila mwezi wa Februari 14, kila mwaka.

Kulingana na Samidoh mwanamke akikualika nyumbani kwake siky ya valentines haya basi hakupendi kwana anataka mpenzi wake akupate hapo.

"Dem akikuita kwake this Valentine huyo hakupendi...anataka upatwe na chali yake akuue😊🤣😆...Chunga sana," Aliandika Samidoh.

Samidoh alivuma sana mwaka jana baada ya kutangaza kwamba anatarajia mtoto na mwanasiasa Karen Nyamu.

Je umeulizwa 'will you be my valentines' ama hupendi vitu vya dunia?